At-Tawba 9:125
التوبةوَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ كَـٰفِرُونَ
Na ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi iliwazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ya kuwa wao ni makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi inawazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ni makafiri. [125]
[125] Ama wanaafiki ambao nyoyo zao zinaugua, na macho yao yamepofoka, hao haziwazidishi ila ukafiri juu ya ukafiri walio nao, na watakufa hali nao ni makafiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama wale ambao wana unafiki na shaka ndani ya nyoyo zao katika dini ya Allah Mtukufu, basi kule kuteremka sura kunawaongezea unafiki na shaka juu ya unafiki na shaka walizokuwa nazo kabla ya hapo. Na hawa wataangamia wakiwa katika hali ya kumkanusha Allah Mtukufu na aya Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net