Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 126

At-Tawba 9:126

التوبة

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِى كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ

Maana

Je, hawaoni ya kwamba wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki. [126]

[126] Je! Hawazingatii wanaafiki vile Mwenyezi Mungu anavyo wapa majaribio kila mwaka mara moja au zaidi, kwa balaa namna mbali mbali, kama kuwakashifu siri zao, na kudhihirisha hali zao na kushindwa na Waumini, na kufichuliwa upotovu wao? Kisha juu ya yote hawaachi hao walio nayo wakatubu, wala hawayakumbuki yanao wapata.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani hawaoni wanafiki kwamba Allah Mtukufu Anawapa mitihani, kwa kuwaletea ukame na matatizo na kwa kuyatoa nje yale wanayoyaficha ya unafiki, mara moja au mara mbili kila mwaka? Kisha wao, pamoja na hayo, hawatubii kutokana na ukafiri wao na unafiki wao, wala hawazingatii wala hawakumbuki aya za Allah Mtukufu wazionazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net