Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 127

At-Tawba 9:127

التوبة

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَىٰكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ ٱنصَرَفُوا۟ ۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ

Maana

Na ikishateremka sura, hutazamana wao kwa wao, (kama kwamba wanasema:) "Je, yuko yeyote anayewaona nyinyi" Kisha huondoka wakaenda. Mwenyezi akaziondoa nyoyo zao kwa kuwa hao ni kaumu wasiofahamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiteremka Sura hutazamana wao kwa wao, (kama kwamba wanasema:) Je! Yuko mtu anakuoneni? Kisha hugeukilia mbali. Mwenyezi amezigeuza nyoyo zao kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu. [127]

[127] Na kadhaalika ikiteremka Sura nao wapo barazani kwa Mtume hukonyezana na kuambiana: Yuko mtu anaye kuoneni? Tena nyoyo zao hukengeuka wasimfuate Mtume wala wasimuamini! Mwenyezi Mungu amewazidisha kupotea kwa vile kushikilia kwao kubaki katika upotovu na kuikataa Haki, kwani watu hawa hawafahamu kitu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iteremshwapo sura, wanafiki huwa wakiashiriana kwa macho, kwa kukataa kuteremka kwake, kucheza shere na kuwa na hasira, kwa yale yaliyoteremka humo ya kutaja aibu zao na matendo yao, kisha wanasema, «Je, kuna yoyote anayewaona mkiondoka kwa Mtume?» Iwapo hakuna yoyote aliyewaona huinuka na kuondoka kwa Mtume, (rehema na amani zimshukie), wakiogopa fedheha. Allah Mtukufu Amezipindua nyoyo zao Ameziepusha na Imani kwa sababu wao hawaelewi wala hawazingatii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net