Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 9 · Aya ya 128

At-Tawba 9:128

التوبة

لَقَدْ جَآءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِٱلْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Maana

Hakika amekwishawajia Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yale yanayowataabisha, anawajali sana, kwa Waumini ni mpole na mwenye kuwarehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana. Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. [128]

[128] Enyi watu! Amekujieni Mtume, binaadamu kama nyinyi kwa umbo lake. Anapata dhiki kwa madhara yanayo kusibuni, ana hamu mwongoke, na mwingi wa huruma na rehema kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika amewajia nyinyi, enyi Waumini, mjumbe atokanae na watu wenu, Azionea uzito shida mlizonazo na masumbuko, ana pupa kwamba muamini na mambo yenu yafaulu na yeye kwa Waumini ni mwingi wa upole na huruma.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

At-Tawba

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net