At-Tawba 9:129
التوبةفَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ حَسْبِىَ ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَهُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ
Kwa hivyo, wakigeuka, basi wewe sema, ”Mwenyezi Mungu ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi ninamtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi. [129]
[129] Basi, ewe Mtume! Wakiipuuza Imani, wakaikataa, wewe usihuzunike kwa mapuuza yao. Wewe tafakhari na utukufu wa Mola wako Mlezi, na useme: Ananitosheleza Mwenyezi Mungu, ambaye hapana mungu asiye kuwa Yeye. Juu yake Yeye tu peke yake mimi nategemea. Na Yeye ndiye Mmiliki wa ufalme wote, Mola Mlezi wa viumbe vyote, na ndiye Mwenye utawala mkuu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi washirikina na wanafiki wakikupa mgongo kwa kuacha kukuamini, ewe Mtume, sema kuwaambia, «Mwenye kunitosha ni Allah Mtukufu; Ananitosheleza yote yanayonitia hamu, hapana muabudiwa yoyote wa haki isipokuwa Yeye, Kwake yeye nimetegemea na Kwake Yeye nimeyategemeza mambo yangu yote. Kwani Yeye Ndiye Mwenye kuninusuru na Mwenye kunisaidia. Na Yeye Ndiye Mola wa Άrsh iliyo kubwa, ambayo ndiyo kiumbe kikubwa kabisa.»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net