Yunus 10:1
يونسالٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْحَكِيمِ
Alif Laam Raa.[1] Hizo ni Aya za Kitabu chenye hekima.
[1] Herufi hizi "Alif Laam Raa" na herufi nyinginezo za mkato zilizo mwanzoni mwa sura mbalimbali zinaonyesha hali ya ushindi wa Qur-ani. Kwani, washirikina walipewa changamoto kwayo, lakini wakashindwa na hawakuweza kuipinga, ilhali inajumuisha herufi hizi zinazounda lugha ya Kiarabu. Kwa hivyo, kutoweza kwa Waarabu kuleta kitu kama hicho - ingawa walikuwa ndio watu wenye ufasaha zaidi - kunaonyesha kwamba Qur-ani ni ufunuo (wahyi) kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitabu chenye Hikima. [1]
[1] Harufi hizi - Alif Lam Raa - ni sawa na A.L.R. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameanzia Sura hii. Na Yeye ndiye anajua muradi wake. Na juu ya hivyo zinaashiria kuwa Qur'ani imeundwa kwa harufi hizi hizi za Alifbete, na nyinyi mmeshindwa kuleta mfano wake! Na kwa harufi hizi za kutamkwa zinawazindua washirikina, wakawa wanasikiliza, ijapo kuwa wanawafikiana kuwa wasizisikilize Aya Tukufu hizi na mfano wake ambazo ni Aya za Qur'ani yenye hikima katika mpango wake na maana zake, na ambayo imekusanya hikima na kila linalo wanafuisha watu katika Dini yao na dunia yao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
(Alif, Lãm, Rã’.) Yametangulia maelezo juu ya herufi zilizotajwa kimkato mwanzo wa sura ya Al- Baqqrah. Hizi ni aya za Kitabu kilichopangwa vizuri ambacho Allah Mtukufu Amekipanga na kukifafanua kwa waja Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net