Yunus 10:2
يونسأَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَآ إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ ٱلنَّاسَ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ مُّبِينٌ
Je, imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, “Waonye watu, na wabashirie wale walioamini ya kuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi?” Wakasema makafiri, “Hakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!”
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mmoja wao kuwa: Waonye watu, na wabashirie wale walio amini ya kuwa watakuwa na cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi? Wakasema makafiri: Hakika huyu ni mchawi dhaahiri! [2]
[2] Haiwafalii watu kustaajabu wakakanusha wahyi wetu tunao mfunulia mtu mmoja wao, naye ni Nabii Muhammad s.a.w., ili awahadharishe watu na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na awape bishara njema wale miongoni mwao walio amini, ya kwamba hapana shaka yoyote wana cheo kitukufu cha juu kwa Mola wao Mlezi. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu haigeuki. Wala haiwafalii hao watu wakanushi kumsema Muhammad, Mtume wetu, kuwa yeye ni mchawi maarufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, lilikuwa jambo la ajabu kwa watu lile la kuteremsha kwetu wahyi wa Qur’ani kwa mtu miongoni mwao anayewaonya mateso ya Allah Mtukufu na kuwapa habari njema wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake kwamba wao watapata malipo mazuri kwa matendo mema waliyoyatanguliza? Alipowajia Mtume wa Allah Mtukufu, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwa wahyi wa Allah Mtukufu na akawasomea, wakanushaji walisema, «Muhammad ni mchawi, na aliyokuja nayo ni uchawi wenye ubatilifu waziwazi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net