Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 3

Yunus 10:3

يونس

إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِنۢ بَعْدِ إِذْنِهِۦ ۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Maana

Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi, anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote isipokuwa baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je, hamkumbuki?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki? [3]

[3] Enyi watu! Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake katika siku sita ambazo kipimo chake hakijui ila Mwenyezi Mungu. Akatandaza utukufu wa utawala wake, peke yake, na akayapanga mambo yote ya viumbe vyake. Basi hapana yeyote mwenye chochote pamoja na utawala wa Mwenyezi Mungu. Wala hawezi yeyote katika viumbe vyake hata kumwombea mtu isipo kuwa kwa ruhusa yake. Huyo, basi, ndiye Mwenyezi Mungu Muumba, huyo ndiye Mola wenu Mlezi, na ndiye Mlinzi wa neema zenu. Basi muabuduni Yeye peke yake, na msadikini Mtume wake, na kiaminini Kitabu chake. Juu yenu kukumbuka neema za Mwenyezi Mungu, na zingatieni Ishara zake zinazo thibitisha Upweke wake. Mwenyezi Mungu ameumba viumbe vyote kwa vipindi sita, na vipindi hivi ni viwango vya mamilioni ya makarne na makarne. Na hivyo ndivyo vinavyo itwa Siku Sita. Na katika kila nguzo za ulimwengu zipo Ishara wazi zilizo zagaa za kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Miongoni mwa hizi, ni hivi kufanywa jua na mwezi na nyota kunyenyekea kwa faida ya binaadamu. Na kadhaalika kupishana zamu usiku na mchana, na kuwa mchana unaingilia kiza cha mbingu. Na umetajwa usiku mbele kwa kuwa kiza ndio asli. Ama mchana umezuka kwa kuathirika kwa mwangaza wa jua katika anga la ardhi, ambayo hiyo ardhi inazunguka wenyewe kwa wenyewe kama pia ili ipate mwangaza wa jua, mara upande huu na mara upande huu

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Mola wenu ni Allah Mtukufu Ambaye Alizipatisha mbingu na ardhi katika kipindi cha Siku Sita, kisha Akawa juu ya ‛Arsh, kulingana na utukufu Wake. Anaendesha mambo ya viumbe Vyake. Hakuna yoyote Anayempinga katika uamuzi Wake na hakuna muombezi yoyote anayeombea mbele Yake Siku ya Kiyama isipokuwa baada ya Yeye kumpa idhini kuombea. Basi muabuduni Allah Mtukufu, Mola wenu, Anayesifika kwa sifa hizi na mtakasieni ibada. Je, hamuwaidhiki na mkazizingatia aya hizi na hoja?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net