Yunus 10:4
يونسإِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُۥ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ بِٱلْقِسْطِ ۚ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ
Kwake Yeye tu ndiyo marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walioamini na wakatenda mema. Na wale waliokufuru, wana vinywaji vya maji ya moto, na adhabu chungu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyakufuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya kweli. Hakika Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe kwa uadilifu wale walio amini na wakatenda mema. Na walio kufuru, wao watapata vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru. [4]
[4] Kama Mwenyezi Mungu alivyo anzisha uumbaji wa viumbe peke yake, basi marejeo yenu, na marejeo ya viumbe vyote ni kwake Yeye. Na Mwenyezi Mungu ameahidi hivyo kwa ahadi ya kweli isiyo na khitilafu. Na hakika Yeye Subhanahu ameanzisha kuumba viumbe kwa kudra yake, na vitapo teketea atavirejesha kwa kudra yake, ili awalipe Waumini wenye kumt'ii thawabu kwa uadilifu ulio timia. Ama makafiri, wao huko katika Jahannamu watapewa vinywaji vinavyo tokota kweli kweli, na watapata adhabu yenye kutia machungu kuwa ni malipo ya ukafiri wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa Mola wenu ndio marejeo yenu nyote Siku ya Kiyama. Na hili ndilo agizo la Allah Mtukufu lililo kweli. Yeye Ndiye Ambaye Anaanza kuumba viumbe kisha Atawarudisha baada ya kufa, Awafanye wawe hai kama walivyokuwa mwanzo, ili Awalipe waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mazuri malipo mazuri zaidi kwa uadilifu. Na wale waliokanusha upweke wa Allah Mtukufu na ujumbe wa Mtume Wake watakuwa na vinywaji vya maji moto sana yanayochoma nyuso na kukata tumbo; na watakuwa na adhabu inayoumiza kwa sababu ya ukafiri wao na upotevu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net