Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 5

Yunus 10:5

يونس

هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ ٱلشَّمْسَ ضِيَآءً وَٱلْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُۥ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا۟ عَدَدَ ٱلسِّنِينَ وَٱلْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ ذَٰلِكَ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Maana

Yeye ndiye aliyelifanya jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo isipokuwa kwa haki. Anazipambanua Ishara kwa kaumu wanaojua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua. [5]

[5] Na Mola wenu Mlezi ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi, na akalifanya jua litoe mwanga, na mwezi utoe nuru. Na akajaalia mwezi uwe na vituo ili vikusaidieni kuweza kupima nyakati zenu, na mjue idadi ya miaka na hisabu. Na wala Mwenyezi Mungu hakuumba hayo ila kwa hikima. Na Yeye Subhanahu katika Kitabu chake anazikunjua Ishara zenye kuonyesha Ungu wake na ukamilifu wa uwezo wake, ili mpate kuzingatia kwa akili zenu, na mkubali kwa yanayo hitajia ujuzi. Aya hii ya 5 inahakikisha ukweli wa kisayansi ambao haukujuulikana na hiyo sayansi ila hivi mwishoni. Hapo kwanza haukujuulikana, nao ni kuwa jua ni umbo lenye kuwaka moto, na ndio chanzo cha nguvu za kufanyia kazi zote, kwa Kiarabu huitwa T'aaqa, na kwa Kiingereza Energy, na kwa Kiswahili cha sasa Nishati. Katika nguvu hizo ni huo Mwangaza na Joto. Ama mwezi hauwaki moto, bali unarudisha mwangaza wa jua, kama kioo, kwa hivyo huonekana una nuru. Kwa hivyo Subhanahu ameeleza kuwa jua lina mwangaza wa asli, na mwezi unatoa nuru tu. Na Aya hii imeashiria hakika ya nyendo za falaki, nayo ni kuwa mwezi unaizunguka ardhi, na kila siku unakuwa katika mahala fulani kwa mintarafu ya dunia. Ukimaliza mzunguko wake ndio unatimia mwezi, huu wa siku 30 au 29. Kwa hivyo tunaweza kujua kiasi cha mwaka, na kwa hivyo twaweza kujua hisabu za miaka, miezi na siku.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Ndiye ambaye Alilifanya jua kuwa dhwiy’a (mwangaza), Akaufanya mwezi kuwa ni nûr (mng’aro) na Akaupangia mwezi njia zake za kupita. Ikawa kwa jua zinajulikana siku, na kwa mwezi inajulikana miezi na miaka. Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Hakuumba jua na mwezi isipokuwa ni hekima kubwa, na kuonesha ukamilifu wa uwezo wa Allah Mtukufu na ujuzi Wake; Anafafanua hoja na dalili kwa watu wanaojua hekima ya utengenezaji wa uumbaji.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net