Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 6

Yunus 10:6

يونس

إِنَّ فِى ٱخْتِلَـٰفِ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ

Maana

Hakika katika kuhitilafiana usiku na mchana, na katika vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa kaumu wamchao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu. [6]

[6] Hakika katika kufuatana usiku na mchana na kukhitalifiana kwao, kwa kuzidi na kupungua, na katika uumbaji wa mbingu na ardhi na vitu vyote viliomo humo, zipo dalili zilizo wazi na hoja zilizo dhaahiri zenye kuhakikisha Ungu wa Mwenye kuumba, na uwezo wake. Hayo ni kwa wenye kutaka kuiepuka ghadhabu yake na wakaiogopa adhabu yake. Aya hii ya 6 inaashiria hakika inayo onekana, nayo kukhitalifiana urefu wa usiku na mchana kwa mwaka mzima katika pahala popote duniani. Na kadhaalika kufuatana mchana na usiku, na kuwa mchana ni wa kuangaza na kuonana, na usiku ni giza. Na maana ya hayo ni kuwa msingi wake ni kuwa dunia inazunguka wenyewe kwa wenyewe kama pia juu ya msumari wake, na vile vile inalizunguka jua. Na yote hayo ni dalili ya uwezo wa Mwenye kuumba katika kuanzisha uumbaji. Ujuzi wa mambo hayo wakati wa Mtume s.a.w. haukuwepo. Na hii ni dalili nyengine ya kwamba haya hayakuwa ila ni wahyi, ufunuo, ulio toka kwa Mwenyezi Mungu kumpa Mtume s.a.w.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika katika kupishana usiku na mchana na Alichokiumba Allah Mtukufu, katika mbingu na ardhi na zilizomo ndani yake zilizopangika na kutengenezeka miongoni mwa maajabu ya uumbaji, ni dalili na hoja zilizo wazi kwa watu wanaoogopa mateso ya Allah Mtukufu, ghadhabu Zake na adhabu Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net