Yunus 10:7
يونسإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا وَرَضُوا۟ بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَٱطْمَأَنُّوا۟ بِهَا وَٱلَّذِينَ هُمْ عَنْ ءَايَـٰتِنَا غَـٰفِلُونَ
Hakika wale wasiotaraji kukutana nasi, na wakaridhia uhai wa dunia hii na wakatua nao, na wale walioghafilika mbali na Ishara zetu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wasio taraji kukutana nasi, na wakaridhia maisha ya dunia na wakatua nayo, na walio ghafilika na Ishara zetu! [7]
[7] Hakika wale wasio amini kufufuliwa na kukutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Mwisho, na wakaamini - kwa kudhani tu - kuwa uhai wa duniani ndio mwisho wao na hapana baada yake uhai mwingine, na wakatulia nyoyo zao kwa hayo, na wala wasijue nini kitakuwa baada yake, na wakaghafilika na Ishara za Mwenyezi Mungu juu ya kufufuliwa na kuhisabiwa,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika ya wale ambao hawana matumaini ya kukutana na sisi Akhera kwa kuhesabiwa na yanayofuatia ya malipo juu ya matendo kwa kuwa wanakanusha kufufuliwa, wakaridhika na maisha ya ulimwenguni kuwa ni badala ya Akhera, wakajitegemeza nao huo ulimwengu, na wale ambao wao ni wenye kughafilika na alama zetu zilizoko ulimwenguni na zilizomo kwenye Sheria.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net