Yunus
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَآ إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ ٱلنَّاسَ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ قَالَ ٱلْكَـٰفِرُونَ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ مُّبِينٌ 2
{2} Na pamoja na haya, wengi wao walipeana mgongo, na wakakosa kujua, basi wakastaajabu, “kwamba tumemfunulia mwanamume kutokana nao kuwa, “Waonye watu” adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wahofishe ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wakumbushe Ishara za Mwenyezi Mungu, na wabashirie “wale walioamini.” Yaani, imani ya ukweli “kuwa wana cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi” yaani, wana malipo mengi, na thawabu zilizohifadhiwa kwa Mola wao Mlezi kwa sababau ya matendo mema na ya ikhlasi waliyoyatanguliza. Basi makafiri wakamstaajabia mwanamume huyu mkubwa kustaajabu kulikowapelekea kumkufuru! Basi "makafiri wakasema" juu yake, “Hakika huyu ni mchawi aliye dhahiri!” Yaani, mwenye uchawi ulio wazi, na haufichiki – kulingana na madai yao – kwa yeyote. Na hili ni katika upumbavu wao na ukaidi wao. Kwani walistaajabu kwa jambo ambalo si la kustaajabisha wala sio geni, bali kunashangaza ujinga wao na kutojua kwao masilahi yao. Vipi hawakumwamini Mtume huyu mtukufu ambaye Mwenyezi Mungu alimtuma kutokana nao wenyewe? Walimjua haki ya kumjua, lakini wakaukataa wito wake na wakawania kuibatilisha dini yake? Na Mwenyezi Mungu ataikamilisha nuru yake, hata kama makafiri watachukia.