Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 74

Al-Anfaal 8:74

الأنفال

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَوا۟ وَّنَصَرُوٓا۟ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Maana

Na wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliotoa pahali pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha (wa Mwenyezi Mungu) na riziki njema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema. [74]

[74] Na walio amini, na wakahajiri, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio wapa makaazi, na wakaisaidia Haki na Neno la Mwenyezi Mungu - hao ndio walio na Imani ya kweli. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawasamehe, na watapata riziki kubwa duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wakaacha majumba yao wakaelekea Nyumba ya Uislamu au kwenye nchi ambayo ndani yake watapata utulivu wa kumuabudu Mola wao, wakapigana jihadi kwa kulikuza neno la Allah Mtukufu, na wale waliowahami ndugu zao Muhãjrûn, wakawapa Makao na wakawaliwaza kwa mali na kwa kuwapa nguvu. Hao basi ndio Waumini wakweli kidhati. Watapata msamaha wa madhambi yao na riziki njema iliyo kunjufu katika mabustani ya Pepo ya starehe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net