Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 73

Al-Anfaal 8:73

الأنفال

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِى ٱلْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ

Maana

Na wale waliokufuru ni marafiki walinzi wenyewe kwa wenyewe. Msipofanya hivi, itakuwepo fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa. [73]

[73] Na walio kufuru wao ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Na wao husaidiana kwa mambo ya upotovu, na wanaungana mkono kukufanyieni nyinyi uadui. Basi nyinyi msifanye nao urafiki. Mkikhaalifu, yaani mkenda kinyume na haya mkawafanya ni wenzenu itaingia fitna katika safu zenu, na utakuwa uharibifu mkubwa katika nchi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waliokanusha, ni wenye kusaidiana wao kwa wao. Na iwapo hamtakuwa, enyi Waumini, ni wenye kusaidiana nyinyi kwa nyinyi, basi kutapatikana katika ardhi kufitiniwa Waumini na dini ya Allah Mtukufu na uharibifu mkubwa wa kuzuiwa njia ya Allah Mtukufu na kutiwa nguvu misingi ya ukafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net