Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 72

Al-Anfaal 8:72

الأنفال

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَوا۟ وَّنَصَرُوٓا۟ أُو۟لَـٰٓئِكَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَلَمْ يُهَاجِرُوا۟ مَا لَكُم مِّن وَلَـٰيَتِهِم مِّن شَىْءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا۟ ۚ وَإِنِ ٱسْتَنصَرُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ فَعَلَيْكُمُ ٱلنَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍۭ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَـٰقٌ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Maana

Hakika wale walioamini na wakahama na wakaipigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, na wale waliotoa pahali pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhama, nyinyi hamna wajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa juu ya kaumu ambao lipo agano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema yale mnayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao, na wale walio toa mahala pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walio amini lakini hawakuhama, nyinyi hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda. [72]

[72] Hakika walio isadiki Haki na wakaikubali hukumu yake, wakahama Makka, wakapigana Jihadi kwa mali yao na roho zao, na wale walio wapa makaazi wakimbizi ugenini, wakamsaidia Mtume wa Mwenyezi Mungu, wanapigana vita na wale wanao wapiga vita. Wanamfanyia uadui anao wafanyia uadui. Wao kwa wao wanasaidia kuunga mkono Haki, na kutukuza Neno la Mwenyezi Mungu. Na wale wasio hama, haijathibiti kupata ulinzi na msaada wa Waumini, mpaka wahajiri. Lakini wakikutakeni muwanusuru na wanao wakandamiza katika Dini, basi wanusuruni. Wakikutakeni muwasaidie dhidi ya watu ambao mna mapatano nao, na wala hawakuvunja mapatano hayo, basi msiwakubalie. Na Mwenyezi Mungu anayaona myatendayo, hana kinacho fichika kwake. Basi simameni kwenye mipaka yake msije mkatumbukia katika adhabu yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao wamemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakazifuata sheria Zake kivitendo, wakahama kwenda kwenye Nyumba ya Uislamu au nchi ambayo wataweza hapo kumuabudu Mola wao, wakapigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu kwa mali na nafsi, na Wale ambao waliowaweka Wahamiaji katika nyumba zao, wakawaliwaza kwa mali yao na wakaitetea dini ya Allah Mtukufu, hao ni wenye kusaidiana wao kwa wao. Ama wale walioamini na wasihame kutoka kwenye Nyumba ya ukafiri, basi nyinyi hamlazimishwi kuwahami na kuwatetea mpaka watakapo hama. Na wakifanyiwa maonevu na Makafiri na wakataka msaada wenu, basi wakubalieni, isipokuwa iwapo ni dhidi ya watu ambao kuna makubaliano ya mkazo baina yenu na wao na hawajayavunja. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona matendo yenu, Atamlipa kila mtu kwa kadiri ya nia yake na tendo lake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net