Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 71

Al-Anfaal 8:71

الأنفال

وَإِن يُرِيدُوا۟ خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا۟ ٱللَّهَ مِن قَبْلُ فَأَمْكَنَ مِنْهُمْ ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na ikiwa wanataka kukufanyia hiana, basi hakika walikwishamfanyia hiana Mwenyezi Mungu kabla, naye akawawezesha nyinyi kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana Mwenyezi Mungu kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima. [71]

[71] Na pindi wakitaka kukukhuni, kwa vile baadhi yao walivyo onyesha kumili kwenye Uislamu, pamoja na nyoyo zao kupenda kukufanyia khiana makusudi, wewe usivunjike moyo. Mwenyezi Mungu atakupa uwezo juu yao. Kama hapo kwanza walipo mkhini Mwenyezi Mungu kwa kumfanyia wenzi na washirika wa kuwaabudu, na wakaikufuru neema yake, na Yeye aliwaweza kwa kukupa ushindi juu yao katika Badri, juu ya kuwa jeshi lako ni dogo na lao ni kubwa. Na Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye ushindi, Muendeshaji kwa hikima yake, aliwathibitisha wakawa na nguvu waja wake Waumini kwa nusura yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakitaka kukuendea kinyume mara nyingine, wale uliowaacha huru miongoni mwa mateka, basi usikate tamaa. Kwani wao tangu hapo walikuwa wamefanya uhaini kwa Allah Mtukufu na wakakupiga vita, na Allah Mtukufu Akakupa ushindi juu yao. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani, ni Mwenye hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net