Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 70

Al-Anfaal 8:70

الأنفال

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ قُل لِّمَن فِىٓ أَيْدِيكُم مِّنَ ٱلْأَسْرَىٰٓ إِن يَعْلَمِ ٱللَّهُ فِى قُلُوبِكُمْ خَيْرًا يُؤْتِكُمْ خَيْرًا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Ewe Nabii! Waambie wale walio katika mikono yenu miongoni mwa mateka: Kama Mwenyezi Mungu akijua heri yoyote katika nyoyo zenu, atawapa bora kuliko vilivyochukuliwa kutoka kwenu, na atawasitiria dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi akiona kheri yoyote nyoyoni mwenu atakupeni bora kuliko vilivyo chukuliwa kwenu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [70]

[70] Ewe Nabii! Waambie hao mateka walio angukia mikononi mwenu: Ikiwa katika nyoyo zenu ipo kheri anayo ijua Mwenyezi Mungu, Yeye atakulipeni yaliyo bora zaidi kuliko hicho walicho kichukua Waumini, na atakusameheni ushirikina wenu na madhambi mliyo kuwa nayo. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghfira na rehema kwa mwenye kutubia madhambi yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii, waambie mliowateka siku ya vita vya Badr, Msisikitike juu ya fidia iliyochukuliwa kutoka kwenu. Iwapo Allah Mtukufu Atajua kwamba kwenye nyoyo zenu pana wema, basi Atawapa kilicho bora zaidi kuliko mali yaliyochukuliwa kutoka kwenu, kwa kuwarahisishia nyinyi, kwa hisani Yake, wema mwingi - Allah Mtukufu Alitekeleza ahadi Yake kwa Abbãs, (Allah Mtukufu Awe radhi naye,) na wengineo- na Atawasamehe madhambi yenu. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha wa madhambi ya waja Wake wanapotubia, ni Mwenye huruma kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net