Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 69

Al-Anfaal 8:69

الأنفال

فَكُلُوا۟ مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَـٰلًا طَيِّبًا ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Basi kuleni katika mlivyoteka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [69]

[69] Basi sasa tumieni mlicho kipata katika fidia kwa kuwa ni halali kwenu, wala si uchumi muovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kusamehe na kumrehemu amtakaye katika waja wake pindi akirejea.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni mlichokipata katika ngawira na fidia ya mateka, kwani hiyo ni halali nzuri. Na jilazimisheni na hukumu za Allah Mtukufu na sheria Zake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake, ni Mwenye huruma nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net