Al-Anfaal 8:68
الأنفاللَّوْلَا كِتَـٰبٌ مِّنَ ٱللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَآ أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Lau lisingelikuwa andiko lililokwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ingewagusa adhabu kubwa kwa vile mlivyochukua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lau isingeli kuwa hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingeli kupateni adhabu kubwa kwa vile mlivyo chukua. [68]
[68] Ingeli kuwa hapana hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumsamehe mwenye kujitahidi japo kuwa amekosa, basi ingeli kupateni adhabu kubwa kwa papara mliyo ifanya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lau si Kitabu kutoka kwa Allah Mtukufu chenye mapitisho na Makadirio yaliyotangulia ya kuhalalisha ngawira na kukomboa mateka kwa ummah huu, basi ingaliwapata adhabu kubwa kwa kuchukua kwenu ngawira na fidia kabla ya kuletwa sheria kuhusu mambo mawili hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net