Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 67

Al-Anfaal 8:67

الأنفال

مَا كَانَ لِنَبِىٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنْيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلْـَٔاخِرَةَ ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Maana

Haikuwa kwa Nabii yeyote kwamba awe na mateka, mpaka awe ameshinda sawasawa katika ardhi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda baraabara katika nchi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima. [67]

[67] Haimfalii Nabii yeyote kukamata mateka, au kuchukua fidia, au kutoa bure msamaha, mpaka ashinde, na maadui waone wameshindwa, na wawe wamepata pigo kubwa hata kuwa hawawezi tena kupigana katika nchi. Lakini, nyinyi jamaa wa Kiislamu, mmefanya haraka katika Vita vya Badri kukamata mateka kabla hamjatamakani mkawa imara katika nchi. Mnatafuta manufaa ya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera, kwa kutukuzwa Neno la Haki, na lisikushughulisheni la dunia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda. Hukupangieni mambo yenu kwa mujibu wa faida yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Haifai kwa Nabii awe na mateka miongoni mwa maadui wake mpaka auwe kwa wingi, ili kutia hofu ndani ya nyoyo zao na aimarishe misingi ya Dini. Mnataka, enyi mkusanyiko wa Waislamu, kwa kuchukuwa kwenu fidia kutoka kwa mateka wa vita vya Badr, starehe ya ulimwenguni, na Allah Mtukufu Anataka kuikuza dini Yake ambayo kwayo hupatikana Akhera. Allah Mtukufu ni Mshindi Asiyeshindwa, ni Mwingi wa hekima katika sheria Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net