Al-Anfaal 8:66
الأنفالٱلْـَٔـٰنَ خَفَّفَ ٱللَّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّا۟ئَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا۟ مِا۟ئَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوٓا۟ أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ ٱللَّهِ ۗ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّـٰبِرِينَ
Sasa Mwenyezi Mungu amewapunguzia, na alijua kuwa ndani yenu upo udhaifu. Kwa hivyo, wakiwapo watu mia moja miongoni mwenu wenye kusubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja, watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri. [66]
[66] Ilivyo kuwa ni waajibu wenu enyi Waumini, kusubiri mnapo kutana na maadui zenu katika hali ya kuwa mna nguvu, ijapo kuwa wamekuzidini mara kumi, sasa Mwenyezi Mungu amekuruhusini katika hali isiyo kuwa ya nguvu, kuwa mvumilie ikiwa adui kakuzidini mara mbili basi. Hayo ni kwa kukujua kwake kuwa hamna nguvu nyingi, kwa hivyo mmefanyiwa wepesi na mmesahilishiwa, baada ya kuwa heba ya Uislamu imeingia katika nafsi za makafiri. Kwa hivyo mkiwa nyinyi ni wapiganaji mia wenye kusubiri mnaweza kuwashinda makafiri mia mbili. Na mkiwa elfu moja mtawashinda elfu mbili, kwa Mwenyezi Mungu kupenda na kusaidia. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri kwa nusura yake na kuunga mkono kwake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sasa hivi Allah Mtukufu Amewapunguzia, enyi Waumini, kwa udhaifu mlio nao. Basi ikiwa watakuwako miongoni mwenu watu mia moja wenye subira, watawashinda Makafiri mia mbili. Na iwapo watakuwako kati yenu watu elfu moja, watawashinda watu elfu mbili kati yao kwa matakwa ya Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu Yuko pamoja na wenye subira kwa msaada Wake na nusura Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net