Al-Anfaal 8:65
الأنفاليَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ حَرِّضِ ٱلْمُؤْمِنِينَ عَلَى ٱلْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَـٰبِرُونَ يَغْلِبُوا۟ مِا۟ئَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّا۟ئَةٌ يَغْلِبُوٓا۟ أَلْفًا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ
Ewe Nabii! Wahimize Waumini juu ya kupigana vita. Wakiwapo miongoni mwenu ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo miongoni mwenu mia, watawashinda elfu moja katika wale waliokufuru, kwa sababu wao ni kaumu wasiofahamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu. [65]
[65] Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani kwa ajili ya kulinyanyua Neno la Mwenyezi Mungu, na wapendezeshe kwa yatayo wafwatia katika kheri ya dunia na Akhera watayo ipata, ili nafsi zao ziingie nguvu. Nayo ikiwa wapo kati yenu watu ishirini walio shikamana na Imani na subira na ut'iifu, basi watawashinda makafiri mia mbili. Hayo ni kwa sababu wao ni watu wasio fahamu ukweli wa mambo, kwani hawana Imani, wala subira, wala tamaa ya kupata thawabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Nabii, wahimize wanaokuamini kupigana vita. Iwapo watapatikana kati yenu watu ishirini wenye kusubiri kwenye kipindi cha kupambana na adui, watawashinda watu mia mbili kati yao. Na iwapo watapatikana kati yenu wapiganaji jihadi mia moja wenye subira, watawashinda Makafiri elfu moja, kwa kuwa wao ni watu wasiokuwa na ujuzi na ufahamu wa yale ambayo Allah Mtukufu Amewaandalia wapiganaji jihadi katika njia Yake; kwani wao wapigania utukufu katika ardhi na kufanya uharibifu ndani yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net