Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 64

Al-Anfaal 8:64

الأنفال

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ حَسْبُكَ ٱللَّهُ وَمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutosha wewe na mwenye kukufuata miongoni mwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na Waumini walio kufuata. [64]

[64] Ewe Nabii! Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kukudhamini wewe na wenye kukufuata miongoni mwa Waumini katika kila jambo lenye maana kwenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe Nabii, hakika Allah Mtukufu Atakukinga wewe na Atawakinga wale walio pamoja na wewe shari ya maadui wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net