Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 63

Al-Anfaal 8:63

الأنفال

وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ ۚ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا مَّآ أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Maana

Na akaziunga pamoja nyoyo zao. Lau wewe ungelitoa vyote vilivyo katika ardhi, usingeliweza kuziunga pamoja nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [63]

[63] Na Mwenyezi Mungu akawaweka pamoja kwa mapenzi baada ya mtafaruku na uadui, hata wakawa marafiki mbele yako, wakizisabilia roho zao na mali yao kwa ajili ya wito wako. Na wewe hata ungeli toa mali yote na vitu vyote vya nafuu viliomo duniani kwa ajili ya kuwaunga pamoja huku, usinge weza kuyapata hayo. Kwa sababu nyoyo zimo katika mkono wa Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye aliye waunganisha, kwa kuwaongoa kwenye Imani na mapenzi na udugu. Hakika Yeye Mtukufu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Anawapangia waja wake kwa mujibu wa manufaa yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

na Akaziweka pamoja nyoyo zao baada ya utengano, lau ungalitoa mali yaliyoko duniani kote hungaliweza kuziweka pamoja, lakini Allah Mtukufu Aliziweka pamoja juu ya Imani wakawa ni ndugu wanaopendana. Hakika Yeye ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwenye hekima katika mambo Yake na uendeshaji Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net