Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 62

Al-Anfaal 8:62

الأنفال

وَإِن يُرِيدُوٓا۟ أَن يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ ٱللَّهُ ۚ هُوَ ٱلَّذِىٓ أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِۦ وَبِٱلْمُؤْمِنِينَ

Maana

Na wakitaka kukufanyia hiana, basi hakika Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Yeye ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake, na kwa Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakitaka kukukhadaa basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye aliye kuunga mkono kwa nusura yake na kwa Waumini. [62]

[62] Ikiwa hao maadui wanataka kukukhadaa na kukufanyia ujanja kwa hivyo kuonyesha kuwa wanataka amani, basi Mwenyezi Mungu anakutosheleza kukulinda na vitimbi vyao kwa kila upande. Kwani Yeye alikwisha tangulia kukuunga mkono kwa kukupa ushindi pale alipo kutengenezea sababu zilizo onekana na za siri za kutia imara nyoyo za Waumini katika Wahajiri, wahamiaji walio toka Makka, na Ansari, wasaidizi wa Madina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi wakitaka kukufanyia njama, Allah Mtukufu Atakukinga na udanganyifu wao. Yeye Ndiye Aliyekuteremshia ushindi na Akakutia nguvu kwa Waumini miongoni mwa Muhãjirûn (waliohamia Madina kutoka Makka) na Anṣãr (wenyeji wa Madina)

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net