Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 61

Al-Anfaal 8:61

الأنفال

وَإِن جَنَحُوا۟ لِلسَّلْمِ فَٱجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Na wakiielekea amani, basi nawe pia ielekee, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. [61]

[61] Maadui wakielekea kutaka amani na kuacha uadui wao, basi nawe ewe Mtume, elekea kwenye amani. Kwani vita sio lengo, bali wewe unakusudia kujilinda tu na uadui wao na upinzani wao kupinga wito wako. Basi kubali amani, na umtegemee Mwenyezi Mungu, wala usikhofu vitimbi vyao na njama zao! Yeye Subhanahu ni Mwenye kuzisikia njama zao, ni Mwenye kuijua mipango yao. Hapana kinacho fichikana kwake. Huu ni msingi mkuu katika misingi ya Uislamu, Dini ya Salama. Na leo tunasikia kila dola duniani ina nadi Usalama, na kwa hivyo ukaundwa Umoja wa Mataifa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakielekea kuacha vita na wakapendelea kuishi kwa amani na nyinyi, basi nawe elekea huko, ewe Nabii, na uyategemeze mambo yako kwa Allah Mtukufu na uwe na imani na Yeye. Hakika Yeye Ndiye Mwenye kuyasikia maneno yao, Mwenye kuzijua nia zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net