Al-Anfaal 8:75
الأنفالوَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنۢ بَعْدُ وَهَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ مَعَكُمْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ مِنكُمْ ۚ وَأُو۟لُوا۟ ٱلْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِى كِتَـٰبِ ٱللَّهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۢ
Na wale walioamini baadaye, na wakahama, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni miongoni mwenu. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana zaidi wenyewe kwa wenyewe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu. [75]
[75] Na walio amini baada ya wale wa mwanzo, na mwishoe wakahama nao, na wakapigana Jihadi pamoja na walio tangulia, basi hao ni katika nyinyi, kwa mkusanyiko wa Muhaajirina (Walio hama Makka) na Ansari (walio msaidia Mtume, watu wa Madina). Hao wanastahiki ulinzi na haki kama ziliopo baina ya nyinyi kwa nyinyi. Na walio kuwa wame nasibiana katika Waumini - juu ya urafiki wa Imani -wana urafiki zaidi wa kuwa ni jamaa. Basi hao wanazidiana katika mapenzi, na mali, na kusaidiana, na kuungana mkono. Na Mwenyezi Mungu ameyabainisha hayo katika Kitabu chake. Naye ni Mwenye kujua kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale walioamini, baada ya hawa Muhãjirûn na Anṣãr, wakahama kwenda madina na wakapigana jihadi pamoja na nyinyi katika njia ya Allah Mtukufu, basi hao ni katika nyinyi, enyi Waumini; wana haki mlizonazo nyinyi na wana majukumu mliyonayo. Na wenye ujamaa, kwenye hukumu ya Allah Mtukufu, baadhi yao wanapewa kipaumbele kwa wengine katika kurithiana kuliko Waislamu wa kawaida. Hakika Allah Mtukufu kwa kila kitu ni Mjuzi, Anayajua yanayowafaa waja Wake kuhusu kurithiana wao kwa wao kwa ujamaa na nasaba na kutorithiana kwa mapatano ya kujihami na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yaliyokuwa mwanzo wa Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net