Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 53

Al-Anfaal 8:53

الأنفال

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِّعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَىٰ قَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ ۙ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Hiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuibadilisha neema aliyowaneemesha kwayo kaumu, mpaka wao wabadilishe yale yaliyo katika nafsi zao, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Mwwnyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [53]

[53] Na huu ni uadilifu katika kulipa, kwa sababu Mwenyezi Mungu hakika haibadilishi neema anayo waneemesha watu, kama vile neema ya amani, kutononoka, na afya, mpaka wao wenyewe waigeuze hali yao na sababu zake! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia wayasemayo, na Mwenye kuyajua wayatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Malipo hayo maovu ni kwamba Allah Mtukufu pindi Anapowaneemesha watu neema yoyote, hawaondolei mpaka wabadilishe hali yao njema iwe mbovu, na kwamba Allah Mtukufu ni Mwenye kuzijua hali zao, kwa hivyo huwapitishia yale yaliyolingana na ujuzi Wake na matakwa Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net