Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 52

Al-Anfaal 8:52

الأنفال

كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ ۙ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Maana

Kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawachukua kwa madhambi yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kama ada ya watu wa Firauni na walio kuwa kabla yao - walizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa sababu ya madhambi yao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na mkali wa kuadhibu. [52]

[52] Hakika ada ya hawa washirikina, na shani yao katika ukafiri, ni kama shani ya Mafirauni na majabari wote walio baki walio kuwa kabla yao. Walizipinga Ishara za Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu aliwaadhibu kwa madhambi yao. Wala Yeye si mwenye kuwadhulumu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu katika kutekeleza hukumu yake, na Mkali wa kumlipa anaye stahiki adhabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika yale yaliyowapata washirikina siku hiyo ndio mwendo wa Allah Mtukufu katika kuwatia adabu wakiukaji mipaka miongoni mwa ummah waliotangulia, mfano wa Fir‛awn na waliomtangulia, walipowakanusha Mitume wa Allah Mtukufu na wakazipinga Ayah Zake. Kwa hakika Allah Mtukufu Aliwateremshia mateso Yake kwa sababu ya madhambi yao. Allah Mtukufu ni Mwenye nguvu Asiyeshindwa, ni Mkali wa mateso kwa aliyemuasi na asitubie kutokana na dhambi zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net