Al-Anfaal 8:51
الأنفالذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّـٰمٍ لِّلْعَبِيدِ
Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yenu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono yenu, na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja. [51]
[51] Na hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja wake kwa kuwaadhibu kwa madhambi waliyo yatenda. Bali huo ni uadilifu, kwa sababu hawawi sawa muovu na mwema. Basi kuadhibiwa kwake ni kwa vitendo viovu alivyo vitenda mwenyewe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Malipo hayo ambayo yamewapata nyinyi, enyi washirikina, ni kwa sababu ya matendo yenu maovu katika maisha yenu ya duniani. Na Allah Mtukufu hamdhulumu yoyote, kati ya viumbe Wake, kitu chochote hata kadiri ya uzito wa mdudu chungu. Bali Yeye Ndiye Mwamuzi Muadilifu Asiyedhulumu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net