Al-Anfaal 8:50
الأنفالوَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ يَتَوَفَّى ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۙ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَـٰرَهُمْ وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ
Na laiti ungeliona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, (na kuwaambia), "Ionjeni adhabu iunguzayo!"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto! [50]
[50] Na lau kuwa unaona, ewe Mtume, kile kitisho kikubwa, kinacho wateremkia hawa makafiri, wakati ule Malaika wanapo wafisha na kuwang'oa roho zao, nao wakiwapiga mbele na nyuma, na wakiwaambia: Onjeni adhabu ya Moto kwa sababu ya vitendo vyenu viovu!!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau ingalionekana, ewe Mtume, hali ya Malaika ya kuzichukua roho za Makafiri na kuzitoa, na huku wao wanawapiga nyuso zao wakiwaelekea, na wanawapiga migongo yao wakiwakimbia na wanawaambia, «Onjeni adhabu inayounguza», ungaliona jambo kubwa. Na msururu huu wa maneno ingawa sababu yake ni vita vya Badr, lakini unakusanya hali ya kila kafiri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net