Al-Anfaal 8:49
الأنفالإِذْ يَقُولُ ٱلْمُنَـٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَـٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمْ ۗ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Waliposema wanafiki, na wale wenye ugonjwa katika nyoyo zao, "Watu hawa dini yao imewadanganya." Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima. [49]
[49] Na kumbuka ewe Mtume! Walipo sema wanaafiki miongoni mwa makafiri na wale wenye Imani dhaifu walipo kuoneni mmesimama imara: Hawa Waislamu wameghurika kweli na dini yao! Na hakika mwenye kumwakilisha Mwenyezi Mungu jambo lake, na akamuamini Yeye, na akamtegemea Yeye, basi hapana shaka kuwa Mwenyezi Mungu atamkifia amwondolee hamu yake, na atamnusuru na maadui zake. Kwani hakika Mwenyezi Mungu madaraka yake yana nguvu, naye ni Mwenye hikima katika mipango yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni waliposema watu wenye shaka na unafiki na wagonjwa wa nyoyo, huku wauona uchache wa Waislamu na wingi wa maadui wao, «Imewadanganya hawa Waislamu dini yao, ndipo ikawaingiza kwenye matatizo haya.» Na hawa wanafiki hawakuelewa kwamba mwenye kumtegemea Allah Mtukufu na akawa na uhakika wa ahadi Yake, basi Allah Mtukufu Hatamuacha. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye ushindi, hakuna chochote kinachomshinda, ni Mwenye hekima katika uendeshaji Wake mambo na utengezaji Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net