Al-Anfaal 8:48
الأنفالوَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَعْمَـٰلَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلْيَوْمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّى جَارٌ لَّكُمْ ۖ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّنكُمْ إِنِّىٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ ۚ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ
Na wakati Shetani alipowapambia vitendo vyao, na akasema, "Hakuna yeyote wa kuwashinda leo hii katika watu, nami hakika ni rafiki mlinzi wenu." Basi yalipoonana makundi mawili hayo, akarudi nyuma juu ya visigino vyake, na akasema, "Hakika mimi niko mbali sana nanyi. Hakika mimi naona msiyoyaona. Hakika mimi ninamhofu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. [48]
[48] Na kumbukeni, enyi Waislamu! Pale Shetani alipo kuja kuwazaini hawa washirikina kwa kuwaonyesha kuwa wayatendayo ni mazuri kwa uchochezi wake, akiwaambia: Hapana mtu ye yote anaye weza kuwashinda. Na akawahakikishia kuwa yeye atawalinda, na kuwanusuru! Yalipo kutana makundi mawili katika vita, vitimbi vyake na uchochezi wake ukavunjika. Akarejea nyuma, na akajitoa nao, akaogopa Mwenyezi Mungu asimuangamize. Na Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni pindi Shetani Alipowapambia washirikina yale waliyoyajia na waliyoyakusudia na akawaambia, «Hamna yoyote Atakayewashinda leo, na mimi ni msaidizi wenu.» Basi yalipopambana makundi mawili: washirikina wakiwa pamoja na Shetani, na Waislamu wakiwa pamoja na Malaika, alirudi nyuma Shetani akienda zake na akasema kuwaambia washirikina, «Mimi ni mwenye kujitenga na nyinyi; mimi nawaona Malaika msiowaona waliokuja kuwasaidia Waislamu. Hakika mimi namuogopa Allah Mtukufu.» Basi akawaacha na akajitenga nao. Na Allah Mtukufu ni Mkali wa mateso kwa aliomuasi na hajatubia toba ya kidhati.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net