Al-Anfaal 8:47
الأنفالوَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ خَرَجُوا۟ مِن دِيَـٰرِهِم بَطَرًا وَرِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
Wala msiwe kama wale waliotoka katika majumba yao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na wakiwazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameyazingira yote wanayoyafanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiwe kama wale walio toka majumbani mwao kwa fakhari na kujionyesha kwa watu, na wakawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameyazunguka yote wanayo yafanya. [47]
[47] Wala msiwe kama wale walio toka kwenye majumba yao, nao wana ghururi (udanganyifu) kwa nguvu na neema walizo nazo, wakijifakhari na kujionyesha mbele za watu, wakitaka wasifiwe kwa ushujaa na ushindi, na wao huku wanapinga watu katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaupinga Uislamu. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitendo vyao kwa ujuzi na uwezo. Na Yeye atakuja walipa duniani na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Msiwe kama mfano wa washirikina ambao walitoka nchini mwao kwa majivuno na kujionyesha ili wawazuie watu wasiingie kwenye dini ya Allah Mtukufu. Na Allah Mtukufu kwa wanayoyafanya ni Mwenye kuyazunguka. Hakifichiki Kwake chochote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net