Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 54

Al-Anfaal 8:54

الأنفال

كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ ۙ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَـٰهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَآ ءَالَ فِرْعَوْنَ ۚ وَكُلٌّ كَانُوا۟ ظَـٰلِمِينَ

Maana

Ni kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikadhibisha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawaangamiza kwa madhambi yao, na tukawazamisha watu wa Firauni. Na kila mmoja wao walikuwa madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni kama ada ya watu wa Firauni na walio kabla yao - walizikanusha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawateketeza kwa madhambi yao. Na tukawazamisha watu wa Firauni. Na wote walikuwa wenye kudhulumu. [54]

[54] Kama ilivyo kuwa ada yao na mtindo wao hawa katika kuzikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na neema zake ni kama mtindo wa watu wa Firauni na walio watangulia, hali kadhaalika ada yao na shani yao katika kuendelea kuwakadhibisha Mitume wake, na dalili za Unabii wao, ni kama ada ya watu wa Firauni na walio kabla yao. Basi wamefanana hao katika kukanusha Ishara, na kuupinga Utume wa Mitume, na kuwakadhibisha, na kuendelea juu ya mwendo huo vile vile. Na kila mmoja Mwenyezi Mungu amemtia mkononi kwa dhambi zake -wale kwa midharuba, na vimbunga, na kadhaalika; na watu wa Firauni kwa kuwazamisha. Na wote walikuwa ni madhaalimu wa nafsi zao. Kwa hivyo walistahiki adhabu iliyo wafika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hali ya Makafiri hawa ni kama hali ya Makafiri wa jamaa za Fir‛awn ambao walimkanusha Mûsã, na ni kama hali ya wale waliowakanusha Mitume wao miongoni mwa watu waliopita. Allah Mtukufu Aliwaangamiza kwa sababu ya madhambi yao na Akawazamisha jamaa za Fir‛awn baharini. Na kila ummah kati yao walikuwa wanatenda mambo ambayo haikufaa wao kuyatenda, ya kukanusha kwao Mitume wa Allah Mtukufu na kupinga kwao ayah za Allah Mtukufu na kushirikisha kwao, katika ibada, asiyekuwa Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net