Al-Anfaal 8:55
الأنفالإِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Hakika waovu zaidi ya wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale waliokufuru, basi hao hawaamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika vinyama vilio viovu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao kufuru, basi hao hawaamini; [55]
[55] Hakika katika vyote vilio enea juu ya uso wa ardhi walio waovu mno mbele ya Mwenyezi Mungu katika hukumu yake na uadilifu wake, ni makafiri walio kakamia juu ya ukafiri wao,
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wabaya mno wa wale wanaotembea juu ya ardhi mbele ya Allah Mtukufu ni Makafiri wanaoendeleza ukafiri; wao hawawaamini Mitume wa Allah Mtukufu, hawaukubali upweke Wake wala hawazifuati sheria Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net