Al-Anfaal 8:56
الأنفالٱلَّذِينَ عَـٰهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِى كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لَا يَتَّقُونَ
Wale ambao miongoni mwao ulifanya agano nao, kisha wanavunja agano lao katika kila mara, wala wao hawamchi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila mara, wala hawamchi Mungu. [56]
[56] Nao ni wale ulio fungamana nao kwa mikataba, nao wakawa hawaachi kuivunja kila mara; na watu hao ni Mayahudi ambao hawachelei utukufu wa Mwenyezi Mungu, wala hawakhofu kupatilizwa naye, wala adhabu yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Miongoni mwa wabaya hao ni Mayahudi ambao waliingia pamoja na wewe katika mapatano kwamba hawatakupiga vita wala hawatamsaidia yoyote dhidi yako, kisha wanazivunja ahadi zao mara kwa mara hali ya kuwa wao hawamuogopi Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net