Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 57

Al-Anfaal 8:57

الأنفال

فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِى ٱلْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ

Maana

Kwa hivyo, ukiwakuta katika vita, basi wakimbize kwa hawa wale walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka. [57]

[57] Basi ewe Mtume! Ukiwakuta hawa wavunjao mapatano, na ukasadifiana nao katika vita nawe umeshinda, basi watishe baraabara kwa kuwapa adhabu ya kuwatia uchungu na kuwaogopesha wale walio nyuma yao, upate kuwafarikisha walio baki. Mateso haya ndiyo ya kuwakumbusha uovu wa kuvunja mapatano, na kuwazuia wenginewe wasitende kama hayo. Katika Aya tukufu hizi tunahadharishwa na wale wanao toa ahadi na kisha wakazivunja. Hawa yafaa wapewe adhabu ya kutia mfano kwao na kwa walio nyuma yao. Na katika Aya hii unabainishwa umuhimu wa kuvuruga askari wa adui walio nyuma. Hizi ni mbinu za vita za kisasa, kwani kuzua vurugo katika askari wa nyuma hutosha kuleta fujo na kupelekea jeshi kutawanya askari wake kulinda mgongo wake, na kwa hivyo zinavunjika nguvu zake. Juu ya hivyo katika sehemu za nyuma katika midani ndio huwapo mambo yaliyo khusu idara ya jeshi ambayo juu yake ndio jeshi linategemea kwa msaada. Ukileta vurugu hapa hupelekea kukosekana nidhamu yote ya jeshi, na kwa hivyo ndio huleta kuemewa na kushindwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Pindi utakapopambana na hawa, wanaovunja ahadi na mapatano, katika vita, wape adhabu ambayo itatia hofu kwenye nyoyo za wegine na itaitawanya mikusanyiko yao, huenda wao wakazingatia wasiwe na ujasiri wa kufanya kama yale waliyoyafanya waliotangulia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net