Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 58

Al-Anfaal 8:58

الأنفال

وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَٱنۢبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَىٰ سَوَآءٍ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْخَآئِنِينَ

Maana

Na ukichelea hiana kwa kaumu fulani, basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wahaini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. [58]

[58] Na ukiona alama za hao watu kutaka kuleta khiana kuvunja maagano yaliyo baina yako na wao, ikate njia yao wasiweze kukukhuni, kwa kuwatangazia wewe kuvunja hayo mapatano, mpaka walijue jambo lako, na wasiweze kukukhuni. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini, wala haridhii kuwa nyinyi msifike kwa sifa yao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ukiogopa, ewe Mtume, hiana ambayo ishara zake zimejitokeza, kutoka kwa kundi lolote, basi watupilie mbali ahadi yao, ili zote pande mbili ziwe zimelingana kwa kujua kwamba hapana tena mapatano baada ya leo. Hakika Allah Mtukufu hawapendi wenye kuenda kinyume na ahadi zao, wavunjaji ahadi na mapatano.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net