Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 59

Al-Anfaal 8:59

الأنفال

وَلَا يَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَبَقُوٓا۟ ۚ إِنَّهُمْ لَا يُعْجِزُونَ

Maana

Wala kamwe wasidhanie wale waliokufuru kwamba wao wametangulia mbele. Hakika, wao hawatashinda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele. La, wao hawatashinda. [59]

[59] Wala wasidhani walio kufuru kuwa wamekwisha tangulia na wameiepuka adhabu ya kukhuni kwao na kwenda kinyume! Wao kabisa hawatamshinda Mwenyezi Mungu asiwazunguke na kuwatia nguvuni, bali Yeye peke yake ni Muweza, na atawalipa kwa nguvu zake na uadilifu wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wasidhanie wale ambao walizikanusha ayah za Allah Mtukufu kwamba wao washapita na washaokoka na kwamba Allah Mtukufu Hawawezi; hakika wao hawatakwepa adhabu ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net