Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 31

Al-Anfaal 8:31

الأنفال

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُنَا قَالُوا۟ قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَآءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَـٰذَآ ۙ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ

Maana

Na wanaposomewa Aya zetu, wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo somewa Aya zetu, wao husema: Tumesikia. Na lau tungeli penda tunge sema kama haya. Haya si chochote ila hadithi za watu wa kale tu. [31]

[31] Na ewe Nabii! Kumbuka inda ya washirikina ulipo kuwa ukiwasomea Aya za Qur'ani Tukufu, nazo ni Ishara zetu. Ujahili wao na ghururi yao iliyo pita kiasi iliwapelekea kusema: Tungeli taka kusema kama isemavyo hii Qur'ani tungeli sema; kwani humu hamna chochote ila visa walivyo viandika watu wa kale!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na pindi wanaposomewa, hawa ambao walimkanusha Allah Mtukufu, aya za Qur’ani tukufu, wao husema 1 Kwa kuwa njama za washirikina zinajulikana na athari yoyote, ndio maana ya kuwa Allah Mtukuf zinashinda zao. kwa ujinga wao na kuikejeli kwao haki, «Tumeshalisikia hili hapo nyuma, na lau tunataka tungalisema maneno yafananayo na hii Qur’ani. Haikuwa Qur’ani hii unayotusomea, ewe Muhammad, isipokuwa ni maneno ya urongo ya watu wa kale».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net