Al-Anfaal 8:30
الأنفالوَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ ٱللَّهُ ۖ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلْمَـٰكِرِينَ
Na walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wapangao vitimbi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango. [30]
[30] Na kumbuka ewe Nabii, neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yako, pale washirikina walipo panga njama kukutia nguvuni - ama wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe mji! Hakika walikupangia mipango miovu! Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alikupangia utokane na shari yao. Na mpango wa Mwenyezi Mungu ndio wa kheri, na una nguvu zaidi, na ndio wenye kushinda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbuka, ewe Mtume, wanapofanya njama washirikina wa Maka wakufunge au wakuue au wakuhamishe kutoka mjini kwako. Wanakufanyia njama, na Allah Mtukufu Aliwarudushia njama zao, ikiwa ni malipo yao, na Allah Mtukufu Anafanya njama; na Allah Mtukufu ni bora wa wenye kufanya njama.(1)
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net