Al-Anfaal 8:29
الأنفاليَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ
Enyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuo, na atawasitiria mabaya yenu, na awafutie dhambi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na atakufutieni makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa. [29]
[29] Enyi mlio isadiki Haki na mkaifuata! Mkizinyenyekea amri za Mwenyezi Mungu kwa siri na dhaahiri, Mwenyezi Mungu atakujaalieni katika nafsi zenu uwezo wa kupambanua baina ya Haki na upotovu, na atakutunukieni ushindi wa kutenga baina yenu na maadui zenu, na atakusitirieni maovu yenu yaondoke, naye akusameheni. Na Yeye Subhanahu daima ni Mwenye fadhila kubwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mlio muamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakazifuata sheria Zake kivitendo, mkimuogopa Allah Mtukufu, kwa kufanya maamrisho Yake na kuepuka makatazo Yake, Atawafanya muwe na upambanuzi baina ya ukweli na urongo, Atawafutia madhambi yenu yaliyopita Hatawaadhibu kwayo. Na Allah Mtukufu ni Mwenye hisani na vipewa vyingi vyenye kuenea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net