Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 28

Al-Anfaal 8:28

الأنفال

وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَآ أَمْوَٰلُكُمْ وَأَوْلَـٰدُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجْرٌ عَظِيمٌ

Maana

Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni mtihani, na kwamba Mwenyezi Mungu ana ujira mkubwa kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa. [28]

[28] Enyi Waumini, wenye kusadiki! Jueni kuwa fitna ya nafsi zenu inatokana na kupita mpaka katika mapenzi yenu kwa watoto wenu na mali yenu. Basi isiwe kupenda kwenu kuyapenda mali na wenenu yakazidi kuliko mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hayo yatakuharibieni mambo yenu. Na jueni kuwa malipo ya Mwenyezi Mungu yanakutosheni kuliko mali na watoto.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mjue, enyi Waumini, kwamba mali yenu ambayo Allah Mtukufu Amewapa jukumu la kuyasimamia, na watoto wenu ambao Allah Mtukufu Amewapa, ni mtihani kutoka kwa Allah Mtukufu na ni majaribio kwa waja Wake, ili Ajue: watamshukuru kwa neema hizo na kumtii au watashughulika nazo wamsahau Yeye? Na jueni kwamba mbele ya Allah Mtukufu kuna heri na thawabu kubwa kwa anayemcha na kumtii.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net