Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 27

Al-Anfaal 8:27

الأنفال

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَخُونُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ وَتَخُونُوٓا۟ أَمَـٰنَـٰتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Msimhini Mwenyezi Mungu na Mtume, na mkahini amana zenu, hali ya kuwa mnajua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana zenu, nanyi mnajua. [27]

[27] Enyi mlio isadiki Haki mkaifuata! Haikufaliini kumkhini Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kufanya urafiki na maadui wa Haki, na kukhuni katika ngawira, au kwa kuacha kwenda kwenye Jihadi. Wala msikhuni amana mnazo pewa nanyi mnajua amri na makatazo yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, msimfanyie khiana Allah Mtukufu na Mtume Wake kwa kuyaacha Aliyowalazimisha nayo na kuyafanya Aliyowakataza nayo, na wala msifanye kasoro katika yale ambayo Allah Mtukufu Aliwaamini nayo, na hali nyinyi mnajua kwamba ni amana inayopasa kutekelezwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net