Al-Anfaal 8:26
الأنفالوَٱذْكُرُوٓا۟ إِذْ أَنتُمْ قَلِيلٌ مُّسْتَضْعَفُونَ فِى ٱلْأَرْضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ ٱلنَّاسُ فَـَٔاوَىٰكُمْ وَأَيَّدَكُم بِنَصْرِهِۦ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Na kumbukeni mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa katika ardhi, mkiogopa kwamba watu watawanyakua, naye akawapa pahali pazuri pa kukaa, na akawaunga mkono kwa nusura yake, na akawaruzuku katika vilivyo vizuri ili mshukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, mkionekana wanyonge katika nchi, mnaogopa watu wasikunyakueni, naye akakupeni pahala pazuri pa kukaa, na akakutieni nguvu kwa nusura yake, na akakupeni riziki nzuri ili mpate kushukuru. [26]
[26] Na hebu kumbukeni, enyi Waumini, katika hali ya kuwa mna nguvu, pale mlipo kuwa wachache na wanyonge. Maadui walikudhilini kwa unyonge wenu, nanyi mlishikwa na khofu wasije maadui zenu kukunyakueni. Basi tena mkahama kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yenu yakawa Yathrib (Madina). Na mkapata manusura kwa msaada wa Mwenyezi Mungu na tawfiki yake, na akakuruzukuni ngawira njema kutaraji mtashukuru kwa neema hii, na muendelee katika Njia ya Jihadi kulinyanyua Neno la Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni, enyi Waumini, neema za Allah Mtukufu juu yenu mlipokuwa ndani ya Makka ni wachache wa idadi mnanyanyaswa, mnaogopa msije mkanyakuliwa na makafiri kwa haraka, Akawapatia makao ya nyinyi kuhamia nayo ni Madina na akawapa nguvu kwa kuwapa ushindi juu yao siku ya Badr na Akawapa vyakula kati ya vitu vizuri ambavyo ngawira ni miongoni mwavyo, ili mumshukuru Yeye kwa alichowaruzuku nacho na kuwaneemesha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net