Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 32

Al-Anfaal 8:32

الأنفال

وَإِذْ قَالُوا۟ ٱللَّهُمَّ إِن كَانَ هَـٰذَا هُوَ ٱلْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ ٱلسَّمَآءِ أَوِ ٱئْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Maana

Na waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walipo sema: Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu. [32]

[32] Na kumbuka, ewe Nabii, vipi walivyo kuwa wanakupinga na kumpinga Mwenyezi Mungu hata kwa inda yao wakasema kumwambia Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Ikiwa haya unayo kuja nayo ni mambo madhbuti, basi zijaalie mbingu zitunyeshee mawe, au tuletee adhabu yoyote iliyo kali yenye uchungu!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, neno la washirikina miongoni mwa watu wako wakimuomba Allah Mtukufu, «Iwapo hili alilokuja nalo Muhammad ndio haki itokayo kwako, basi tuteremshie mawe kutoka mbinguni au tuletee adhabu inayoumiza».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net