Al-Anfaal 8:33
الأنفالوَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba msamaha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu nawe umo pamoja nao, wala Mwenyezi Mungu si wa kuwaadhibu na hali ya kuwa wanaomba msamaha. [33]
[33] Si katika hikima ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwaadhibu katika dunia kwa adhabu kali na hali wewe upo miongoni mwao unaitia Haki, nawe unataraji asaa wataitikia. Wala si mtindo wa Mwenyezi Mungu kuwaadhibu wenye kuasi nao wangali wanamuomba maghfira na wamo kuyavua yale waliyo nayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakuwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na sifa za upungufu na kutukuka, ni Mwenye kuwaadhibu washirikina hawa na hali wewe, ewe Mtume, uko pamoja nao, na hakuwa Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaadhibu wao na hali wao wanaomba msamaha wa madhambi yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net