Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 8 · Aya ya 34

Al-Anfaal 8:34

الأنفال

وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ ٱللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَمَا كَانُوٓا۟ أَوْلِيَآءَهُۥٓ ۚ إِنْ أَوْلِيَآؤُهُۥٓ إِلَّا ٱلْمُتَّقُونَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Maana

Lakini wana nini hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu, wala wao hawakuwa ndio walinzi wake? Bali walinzi wake si isipokuwa wacha Mungu tu, lakini wengi wao hawajui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa ndio walinzi wake, bali walinzi wake hawakuwa ila wacha-Mngu tu. Lakini wengi katika wao hawajui. [34]

[34] Hakika hali yao iliyo sasa inaruhusu kuwaadhibu, kwani wanawazuia watu wasiutumie Msikiti ambao Mwenyezi Mungu ameutukuza kwa kuharimisha vita karibu yake. Lakini Mwenyezi Mungu anawaakhirisha kwa alivyo wakadiria katika ujuzi wake kuwa wengi wao watakuja amini. Wao wakati huu wa sasa sio walinzi wa kuunusuru huo Msikiti Mtukufu, bali wao wameunajisi kwa kutia ibada ya masanamu ndani yake. Ama wa kuunusuru hakika ni Waumini, wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu. Lakini wengi katika washirikina hawaijui Dini, wala hawajui cheo cha Nyumba hiyo Tukufu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na vipi wao wasistahili adhabu ya Allah Mtukufu na hali wao wanawazuia mawalii wake Waumini kutufu Alkaba na kuswali ndani ya msikiti wa Harãm. Na wao hawakuwa ni mawalii wa Allah Mtukufu. Mawalii Wake si wengine isipokuwa wale wanaomuogopa Yeye kwa kutekeleza faradhi Alizoziweka na kujiepusha na mambo ya kumuasi. Lakini wengi zaidi wa makafiri hawajui, na kwa hivyo walidai kwamba wana jambo ambalo wasiokuwa wao wana haki nalo zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anfaal

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net